Benki kuu ya Tanzania BOT imetoa mafunzo maalum ya namna bora ya utambuzi wa alama za noti kwa watu wenye ulemavu wa viungo ,wasioona ,viziwi na watu wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na kundi hilo kukubwa na changamoto ya kupambikizwa fedha bandia na kupelekea kudhikumiwa katika biashara zao kwa kutotambua aina ya fedha
Ni mafunzo ya siku tatu yanayotolewa na bank kuu ya Tanzania BOT yaliyoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Social and Economic Empowerment of Disadvantaged Trust (SEED Trust) linalojishughulisha na watu wenye ulemavu mbalimbali kama Wasioona, walemavu wa viungo, viziwi,Albinism na watoto waishio katika mazingira magumu
Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na shirika hilo SEED Trust kupitia mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa fedha kwa watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Morogoro wametuligundua changamoto kwa watu wasioona na wenye uoni hafifu katika kutambua noti na sarafu
ilulu said ilulu ni meneja idara ya sarafu kutoka Bank kuu ya Tanzania BOT amesema lengo la mafunzo hayo kuwajengea uwezo namna bora ya kutambua na matumizi ya alama za nukta nundu kuondokana na changamoto wanazokumbana nazo
“ BOT tumona ni vema tukashirikiana na shilika hili la SEED trust kuwaweza mafunzo haya ya utambuzi wa alama nukta nundu kwa sababu ni kundi kubwa sana linalokumbana na changamoto ya kupambikizwa na hela bandia “
Meya wa manispaa ya Morogoro Mhe pascal Kihanga ndiye mgeni rasmi katika mafunzo hayo ambapo amewataka BOT na shirika hilo kushirikiana kwa karibu kutoa mafunzo kwa nyanja ya vitendo na kuwafikia watu wengi
Msisitizo wa serikali ni wazazi na walezi wenye ulemavu kutotoa ushirikiano wakati Shirika linapotekeleza majukumu yake kama kuwaficha wenye ulemavu husika