Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi alishinda uchaguzi wa rais wa nchi hiyo kwa asilimia 89.6 ya kura, na kujihakikishia muhula mpya wa miaka sita, Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi ilitangaza Jumatatu.
Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hazem Badawy, alisema kuwa idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura imefikia “isiyo na kifani” 66.8% kati ya wapiga kura milioni 67 wa Misri.
Zaidi ya wapiga kura milioni 39 walimpigia kura Bw Sissi ambaye amekuwa akiiongoza nchi kwa muongo mmoja.
Rais alichuana na wagombea watatu: Hazem Omar, kiongozi wa chama cha Republican People’s Party na wa pili katika uchaguzi huo kwa kupata 4.5% ya kura, Farid Zahran, kiongozi wa chama kidogo cha mrengo wa kushoto, na Abdel-Sanad Yamama wa Wafd, chama cha karne lakini sasa cha pembezoni.
Ushindi wa Bw Sissi unamhakikishia muhula wa tatu madarakani, kuanzia Aprili na unaopaswa kuwa wa mwisho kwake, chini ya Katiba ya Misri.
Kuchaguliwa kwake hakukuwa jambo la kushangaza katika nchi yenye watu milioni 106 iliyokumbwa na migogoro mingi, kuanzia katika ununuzi wa madaraka hadi vita katika nchi jirani ya Gaza.
Katikati ya mzozo wa kiuchumi, mfumuko wa bei kwa sasa umefikia 36.4%, wakati sarafu imepoteza nusu ya thamani yake na bei ya baadhi ya vyakula vya msingi inapanda kila wiki.
Theluthi mbili ya watu wanaishi chini au juu ya mstari wa umaskini.
Katika uchaguzi wa urais wa 2014 na 2018, Bw Sisisi alishinda kwa zaidi ya 96% ya kura