Serikali imesema kuwa katika matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022 kwa wadau wote watumie matokeo hayo katika mipango mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi iliyofanyika Mjini Babati.
Twange amesema mafunzo kwa viongozi yana umuhimu katika katika kupanga mipango ya maendeleo kwenye jamii “Sensa iliyofanywa imesaidia ata katika mafuriko yaliyotokea Hanang kutokana na baadhi ya waathirika kuingiza vitu ambavyo havikuwemo na kubaini hayo imetokana na sensa ya mwaka 2022”
Amesema mafunzo hayo wanayoyatoa kwa Makundi mbalimbali yamekuwa na msaada mkubwa kwa watu kwani wamekuwa wakielimisha juu ya uwepo wa ramani ya maeneo yao na kuonyesha kila kitu ambapo inasaidia sasa wananchi kuwajibika kimaendeleo katika maeneo yao.
Mratibu wa Sensa Mkoa Manyara Gidioni Mokiwa amesema katika matokeo hayo NBS imekuwa ikielemisha makundi mbalimbali. Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa mujibu wa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Nae Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo amesema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka katika kwenda kupanga mipango kwenye kuhudumia wananchi wilaya ya Babati.