Timu ya Misitu Fc wametwaa ubingwa wa kombe la Sao Hill Misitu Sports Bonanza kwa mwaka 2023 baada ya kuwafunga kwenye mikwaju ya penati 5-4 timu ya Mgololo Misitu Fc mchezo ambao ulichezwa kwenye dimba la Ihefu lililopo makao makuu ya wakala wa huduma za misitu Tfs ambapo mechi iliisha 1 kwa 1 kwa dk 90 .
Bonanza hilo lilihusisha michezo mbali mbali ikiwemo Draft , mbio ndefu na fupi kukimbia kwenye magunia , kukimbiza kuku , pamoja na mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali Peter Nyehende ambaye ni msaidizi wa mhifadhi mkuu kwa upande wa mipango na masoko amesema lengo la kufanya michezo kwemye shamba hilo ni kuongeza hamasa kwa vijana sambamba na kuongeza elimu kwa wanannchi wanaozunguka misitu hiyo kwenye namna ya kulinda misitu na majanga ya moto pamoja na kuifanya jamii kuwa sehemu ya shighuli za uhifadhi hasa upandaji miti.
Mabingwa wa michuano hiyo ambao ni Misitu Fc wamepata zawadi ya kombe , medali pamoja na fedha taslim shilingi laki 8 ambapo pia mshindi wa pili ambao ni Mgololo Fc walipewa medali pamoja na fedha shilingi laki 6 , na mshindi wa tatu ambao ji Irundi Fc walipata shilingi laki 4 na mshindi wa nne Nundwe Fc walipata zawadi ya mpira mmoja .
Mashindano ya Sao Hill sports Bonanza huandaliwa na kudhaminiwa na wakala wa misitu Tanzania – Tfs kupitia shamba la Misitu Sao Hill na kauli mbiu ya mashindano hayo yalikuwa ni “ panda mti kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi “ yenye lengo ya kuhimiza wanannchi kuhimiza kutumia msimu huu wa mvua zinazonyesha kupanda miti katika maeneo yao .