Raia zaidi ya milioni 40 waliojiandikisha kupiga kura wanakwenda kwenye vituo vya kupigia kura nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuchagua viongazi wao mbalimbali na rais.
Baada ya kampeni za wiki kadhaa, rais Felix Tshisekedi, anagombania muhula mwingine katika uchaguzi ulio na idadi kubwa ya wagombea urais.
DRC kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini hasa usalama upande wa Kaskazini Mashariki, ambapo kuna makundi kadhaa yenye silaha huku kundi la M23 likiendelea kudhoofisha usalama wa eneo hilo.
Kuelekea uchauzi huo, ahadi za kukabiliana na kudhoofu kwa usalama ziligubika kampezi zake, lakini pia masuala mengine kama vile huduma za kijamii ikiwemo afya na hali ya maisha bora kwa raia.
Waandalizi wa uchaguzi wako chini ya shinikizo la kuepuka kurudiwa kwa machafuko ambayo yaliharibu kinyang’anyiro cha mwisho cha urais wa DRC mwaka wa 2018, wakati matatizo ya vifaa, ucheleweshaji na madai ya ulaghai ulioenea vilidhoofisha uaminifu wa kura. Licha ya msukosuko huo, uchaguzi huo ulianzisha kipindi cha kwanza cha mpito wa madaraka kwa amani tangu nchi hiyo ipate uhuru, huku rais wa zamani Joseph Kabila akimkabidhi madaraka mrithi wake Felix Tshisekedi, ambaye anawania muhula wa pili Desemba 20.