Mamlaka yaMapato Tanzania imewataka wafanyabiashara wa vinywaji Mkoani Manyara Kutumia Mfumo wa kieletronoki Kuhakiki Stempu za Kodi Ili kuthibiti Bidhaa Bandia pamoja na biadhaa zinazozalishwa kwenye viwanda Bubu ambayo ni hatarishi Kwa matumizi ya Binadamu.
Akizungumza katika kammpeni ya kuhakiki Stempu inayoendeshwa na Maafisa wa TRA makao majuu, Meneja wa Miradi mfumo wa stempu za kieletroniki (ETS) amesema lengo la mfumo huo ni kudhibiti Biadhaa Bandia pamoja na kuongeza Kodi ya serikali.
“Toka mfumo huu umeanza Tumeweza kudhibiti mizigo ya magendo maana tunajua nchi yetu imepakana na nchi nyingi kwahiyo kabla ya mfumo huu tulikuwa na changamoto kubwa ila sasa Tumeweza kukontro na tuweza kuongeza mapato zaidi”
“niwahamasishe Watanzania wote na watumiaji wa hizi biadhaa ambazo zinatozwa ushuru wa forodha kuwa na utamaduni wa kuhakiki Stempu kabla ya kutumia biadhaa lakini mfumo huu umesaidia kulinda Afya za watumiaji” Abyud Tweve…Meneja Miradi Mfumo wa ETS ,TRA Makao Makuu.
Kwaupande wake Mfanyabiashara wa vinywaji Kutoka Mkoa wa Manyara Richard Peter ameishukuru mamlaka ya mapato Tanzania Mkoa wa Manyara Kwa kuwafikia katika kuwapatia elimu juu ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki Kwa njia ya Simu kwani imekuwa raisi wao kuepukana na usumbufu wa kuuziwa bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda Bubu.