Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa kushirikiana na na taasisi mbaimbali za kiserikali na binafsi limesema limeshakamilisha mchakato wa kuandaa Andiko dhana linaloainisha umhimu wa sekta ya Ujenzi ili kuratibu uandaaji wa Sheria ya Majengo nchini ili kuondoa changamoto zilizopo ikiwemo Majengo kutokuwa na viwango vya Kitaifa vya majengo nchini.
Akizungumza leo Desemba 21, 2023 na Wanahabari Jijini Dodoma Mhandisi Geofrey Ibrahim Mwakasenga Mhandisi Ujenzi katika Baraza la Taifa la Ujenzi NCC. amesema kuwa baadhi ya sheria zinazosimamia ujenzi wa majengo nchini ni pamoja na sheria za mipango miji, sheria ya afya na usalama mahali pa kazi, sheria ya zimamoto na uokoaji, , sheria ya ukandarasi na usajili, sheria ya mazingira, pamoja na sheria zinazosimamia Taaluma na wana taaluma katika fani za uhandisi, ubunifu majengo, na ukadiriaji majenzi.
Mhandisi Geofrey amesema sheria hizo zinatoa mwongozo katika baadhi ya maeneo na kuyaacha mengine bila usimamizi jambo linaloifanya Sekta ndogo ya Ujenzi wa majengo, inayohusisha pia ubomoaji wa majengo kutosimamiwa ipasavyo.
Aidha, Mhandisi huyo ametaja majukumu ya Baraza hilo ambapo mojawapo ni kuhamasisha na kuweka mikakati ya kukuza, kuendeeeleza, na kupanua sekta ya Ujenzi nchini hususani kwa kujenga uwezo na ushindani wa wazawa ili wawezee kushindana na kuteekeleza miradi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akiendelea kutaja majukumu ya Baraza hilo amesema
ni kushauri Serikali juu ya Maendeleo ya Sekta ya Ujenzi nchini na kuandaa Mapendekezo ya utekelezaji wa ushauri huo.
“Kutoa ushauri na msaada wa kitaalamu kwa wadau wa sekta ya ujenzi nchini kuhusu mambo yanayohusiana na sekta ya ujenzi.
Kuratibu na kuendeleza mafunzo Bora kwa wote wanaojihusisha au wanaotarajia kujihusisha na shughuli za ujenzi na shughuli nyingine katika sekta ya ujenzi nchini.” Amesema Mhandisi Geofrey.
Majukumu mengine ni Kufanya, kuhimiza na kuratibu Utafiti katika shughuli zote za sekta ya ujenzi na pia Kuhamasisha na Kufatilia uandaaji na utumiaji wa viwango vya ubora ,kanuni na miongozo mbalimbali inayohusiana na shughuli za Sekta ya ujenzi nchini.
Baraza hilo lipo chini ya Wizara ya Ujenzi