Jeshi la Polisi nchini liseme kuwa hali ya usalama wa nchi ni shwari huku likibainisha kuwa Uhalifu mkubwa na mdogo unaendelea kudhibitiwa kupitia mikakati mbalimbali iliyobuniwa na kuendelea kutekelezwa kwa kushirikisha wananchi na wadau wengine katika kuzuia uhalifu wa kijinai hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime amesema katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Jeshi hilo hilo linapenda kujulisha kuwa limeweka mikakati ya kuhakikisha kila Mkoa na Kikosi unaendeleza mikakati ya kutoa elimu ya kuzuia uhalifu, kufanya misako na operesheni za kuwakamata wale wote watakaovunja sheria.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lingependa kutoa tahadhari kwa wazazi na walezi katika sikukuu hizi kutokuwaruhusu watoto kwenda kwenye maeneo ya mikusanyiko bila uangalizi.
Vilevile ametoa onyo kwa madereva kutokuedesha mwendokasi, vyombo vya moto wakiwa wamekunywa vilevi na kuyapita mara mengine bila ya kuchukua tahadhari.
Sambamba na hilo Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi nchini linawatakia Watanzania wote na wageni watakao kuwepo nchini, heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2024