Malawi imepiga marufuku uingizaji wa mahindi kutoka Kenya na Tanzania kutokana na wasiwasi wa kuenea kwa ugonjwa wa Mahindi Lethal Necrosis ambao kunaweza kuharibu chakula kikuu kinachotegemewa huko.
Zaidi ya watu milioni 4 katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Kenya na Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa vyanzo vikuu vya mahindi kwa Malawi wakati wa vipindi vya uhaba wa chakula.
Hata hivyo, Wizara ya Kilimo ya Malawi ilitangaza marufuku wiki hii ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje katika taarifa inayosema ugonjwa wa Mahindi unaosababishwa na Lethal Necrosis hauna tiba na unaweza kusababisha hasara ya mavuno kwa asilimia 100.
Malawi inakabiliwa na uhaba wa chakula, kwa kiasi kikubwa kutokana na athari za kimbunga Freddy kilichopita mwezi Machi, ambacho kiliharibu maelfu ya hekari za mahindi, zao kuu la chakula nchini humo.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani nchini Malawi na Kamati yaTathmini ya Athari Malawi wanakadiria kuwa watu milioni 4.4, karibu robo ya idadi ya watu nchini humo, watakabiliwa na uhaba wa chakula hadi Machi mwaka ujao.
Serikali ya Malawi inasema marufuku hiyo itakuwa ya muda huku ikichunguza hatua nyingine za kujikinga kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.