Kukamilika kwa kiwanda cha kuzalisha Sukari Mkulazi kilichopo Wilayani kilosa mkoani Morogoro, kumetajwa kuwa kutawezesha kutoa ajira za moja kwa moja na za muda mfupi kwa watu zaidi ya 5000.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Mfuko wa hifadhi wa jamii (NSSF) Mwamini Juma Malemi alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 100 na tayali kimeanza kazi.
Aidha alisema kuwa sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho itaanza kupatikana madukani hivi karibuni na pia kutakuwa na duka maalumu litakalouza sukari Kwa bei elekezi ya kiwanda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Mkulazi Dk. Heridelita Msita alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi na kuwahikishia Watanzania upatikanaji wa sukari ya kutosha kutoka kwenye kiwanda hicho.
Hata hivyo alisema kuwa hadi sasa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiweka oda kwaajiri ya kupata sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho ambacho Kimkuwa na manufaaa makubwa Kwa wananchi na vijana Kwa kupata Ajira na kujiongezea kipato chao.
Ziara hiyo imefanyika lengo likiwa ni kukagua na kujiridhisha namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo Mashamba ya miwa pamoja na Mabwawa kwaajiri ya umwagiliaji.