Serikali inatoa wito kwa wanaowiwa kutoa misaada kwa waathirika wa maafa ya Hanang, kujikita zaidi katika kutoa misaada ya vifaa vya ujenzi.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi kuhusu taarifa ya Serikali juu ya maendeleo ya hali baada ya maafa yaliyotokea wilayani Hanang Mkoa wa Manyara na kueleza kuwa, Serikali imeendelea kupokea na kugawa misaada ya chakula na mahitaji muhimu kwa waathirika wa maafa ya Hanang mkoani Manyara.
“Serikali inawashukuru Watanzania kwa utu, upendo, uzalendo na moyo wa kujitolea ambao umesaidia kupatikana kwa chakula cha kutosha na mahitaji muhimu ili kuwasaidia waathirika kuendelea na maisha yao,” imeeleza taarifa hiyo.