Mashambulio ya anga ya Israel yaliendelea usiku wa Kumapili Desemba 24 kuamkia Jumatatu Desemba 25 kwenye Ukanda wa Gaza, ambapo njaa inatishia wakazi wa eneo hilo. Kwa Wakristo wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, mkesha wa Krismasi mwaka huu umegubika na migogoro, huku Papa Francis akihutubia katika misaa yake kwamba moyo wake unafikiria mji wa Bethlehem.
Waziri Mkuu wa Israel ametangaza tarehe 25 Desemba kuwa amezuru Gaza siku ya Jumatatu na kuahidi kuzidisha mapigano yanayoendelea katika ardhi ya Palestina dhidi ya Hamas. Mbele ya wawakilishi waliochaguliwa wa chama chake, Likud, Benjamin Netanyahu ametangaza: “Sasa ninarejea kutoka Gaza.
Hatusitishi mapigano, tunaendelea kupigana na tutazidisha mapigano siku za usoni na itakuwa ni vita ndefu ambayo haitakwisha hivi karibuni. ”
Leo, wanajeshi wa Israeli wameendeleza mashambulio kwenye ukanda wa Gaza, ambapo watu zaidi ya 70 wameuawa katika Kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi.
Katika hatua nyingine, Misri imetoa pendekezo jipya la usitishaji mapigano hayo ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 20 katika ardhi ya Palestina.