Jumla ya watu 4,139 wamefariki kutokana na ajali za barabarani nchini Kenya mwaka huu.
Mamlaka ya Usalama Barabarani nchini humo (NTSA) imesema, idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na ile ya mwaka 2022, ambapo watu 4,517 walifariki kutokana na ajali za barabarani.
Takwimu zilizotolewa na mamlaka hiyo kuhusu hali ya usalama barabarani mwaka 2023 zimeonyesha kuwa, kwa ujumla, watu 21,684 walihusika kwenye ajali, ambapo watu 10,201 walijeruhiwa vibaya huku wengine 7,344 wakipata majeraha madogo madogo.
Kulingana na takwimu hizo, idadi kubwa ya watu waliofariki ni watembea kwa miguu, wakifuatwa na madereva wa bodaboda.