Papa Francis alitoa baraka zake za Siku ya Krismasi kwa ombi la amani duniani kote, akisisitiza kwamba masimulizi ya Biblia ya kuzaliwa kwa Kristo huko Bethlehemu yanatoa ujumbe wa maelewano.
Mji wa Bethlehem katika ardhi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan umeghairi sherehe nyingi za Krismasi kwa mshikamano na Gaza.
Kwa kawaida Francis anatumia hotuba yake ya kila mwaka kuelezea wasiwasi wake kwa matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia, na mwaka huu pia haukuwa tofauti.
“Tusisahau mivutano na migogoro inayosumbua ukanda wa Sahel, Pembe ya Afrika na Sudan, pamoja na Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini. Siku iwe karibu wakati uhusiano wa kindugu utaimarishwa.
Akizungumzia mizozo kuanzia Armenia na Azerbaijan hadi Syria, Yemen, Ukraine, Sudan Kusini, Kongo na rasi ya Korea, Papa alihimiza juhudi za kibinadamu, mazungumzo, na usalama kushinda ghasia na vifo.
Francis pia aliomba amani ya Palestina na Israeli: “Ninawakumbatia wote, hasa jumuiya za Kikristo za Gaza, parokia ya Gaza, na Ardhi Takatifu nzima. Moyo wangu unahuzunika kwa wahasiriwa wa shambulio la kuchukiza la Oktoba 7 iliyopita, na Nasisitiza ombi langu la dharura la kukombolewa kwa wale ambao bado wanashikiliwa mateka.
Naomba kusitishwa kwa operesheni za kijeshi na mavuno yao ya kutisha ya wahasiriwa wa raia wasio na hatia, na kutoa wito wa suluhisho la hali mbaya ya kibinadamu kwa ufunguzi wa utoaji wa misaada ya kibinadamu.Kuwe na mwisho wa kuchochea ghasia na chuki.
Na swala la Palestina lipate kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo ya dhati na ya kudumu kati ya pande husika, yanayodumishwa na utashi mkubwa wa kisiasa na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.Ndugu na dada. tuombe amani katika Palestina na Israeli,”