Waumini wa kanisa la Orthodox nchini Ukraine wanashehekea Krismasi Desemba 25 kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Ukraine imekuwa ikitumia kalenda ya jadi ya Julian, ambayo pia hutumiwa na Urusi, ambapo Krismasi huadhimishwa Januari 7.
Katika mabadiliko hayo yanayosadikiwa kujitenga na Waorthodox wenzao wa Urusi, sasa Ukraine inaadhimisha Krismasi kulingana na kalenda ya Magharibi – au Gregorian – ambayo hutumiwa katika maisha ya kila siku.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alibadilisha sheria hiyo mwezi Julai, akisema iliwaruhusu raia wa Ukraine “kuacha utamaduni wa Urusi” wa kusherehekea Krismasi mwezi Januari.
Katika ujumbe wa Krismasi uliotolewa Jumapili jioni, Zelensky alisema Waukraine wote walikuwa pamoja na kwa furaha .
“Sote tunasherehekea Krismasi pamoja Katika tarehe moja, kama familia moja kubwa, kama taifa moja, kama nchi moja iliyoungana.”