Mshambulizi wa Manchester City, Julian Álvarez ameashiria kuwa “anafuraha sana” katika klabu ya Manchester City huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha na kuhamia Real Madrid, kwa mujibu wa Daily Mirror.
Alvarez alifunga mara mbili, na kuongeza asisti, katika ushindi wa City wa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Fluminense wiki iliyopita.
Real Madrid ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini Muargentina huyo anasisitiza kuwa anataka tu kuendelea kushinda mataji akiwa na City.
“Ukweli ni kwamba nina furaha sana Manchester City,” Alvarez alisema. “Nimekuwa katika klabu kwa zaidi ya mwaka mmoja. Najisikia furaha sana kwa kila kitu ambacho tumefanikiwa.”