Mradi wa barabara wenye kilometa 4.4 unaounganisha Vijiji viwili vya Itunduma na Kichiwa vilivyopo Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe umetengenezwa kwa zaidi ya milioni 60 kupitia ajira za muda za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Itunduma Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe Shabani Lukelema, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambao wako kwenye ziara yakukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Amesema mradi huo ulianza Novemba 9, 2022 baada ya kuibuliwa na wananchi kwenye mkutano wao kutokana na barabara hiyo kutokuwa rafiki katika matumizi.
“Tunaishukuru sana Serikali kwakutuwezesha fedha kwaajili ya kutengeneza barabara hii,kwa sasa imekuwa rafiki na wananchi wananufaika nayo”, amesema Lukelema.
Kwa upande wake mkazi wa Kijiji cha Itunduma Mary Mfilinge amesema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa kwao ikiwemo kupata ajira ambayo imesaidia kuboresha makazi yao pamoja na kununua mbolea.
“Ajira hii ilikuwani ya masaa manne ukimaliza unaenda kufanya kazi zako za nyumbani kwahiyo umetupa fursa nzuri za kijipatia kipato na kufanya shughuli zetu zingine za uzalishaji”, amesema
Nae Jesca Msigwa amesema awali barabara hiyo ilikuwa inawapa shida hususani kwa wanawake wanapoenda kujifungua kutokana gari kutopita kwa urahisi kurokana na ubovu wa barabara hata hivyo kwa sasa inapitik.