Afisa mkuu wa uchaguzi wa Maine ametoa uamuzi kwamba Donald Trump hawezi kugombea urais mwaka ujao katika jimbo hilo, akinukuu kipengele cha uasi kikatiba.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Shenna Bellows alisema Bw Trump hastahili kwa sababu ya hatua yake iliyosababisha ghasia za Bunge la Marekani mnamo 2021.
Maine sasa inajiunga na Colorado, majimbo hayo mawili ya kumpiga marufuku Bw Trump kuwania urais.
Maamuzi hayo yanaongeza shinikizo kwa Mahakama ya Juu kupima uzito wa hoja hizo.
Uamuzi huo unasema kuwa Bw Trump lazima aondolewe kwenye kura ya Maine kwa sababu ya Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, ambayo yanapiga marufuku mtu yeyote kushikilia wadhifa huo ambaye “amejihusisha na uasi.
Katika agizo lake, Bi Bellows anasema kwamba Bw Trump “katika muda wa miezi kadhaa na kufikia Januari 6, 2021, alitumia simulizi ya uwongo ya udanganyifu katika uchaguzi ili kuwachochea wafuasi wake na kuwaelekeza kwenye Ikulu”.