Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Disemba 29, 2023 amewasili katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ambapo amewashukuru na kuwapongeza kwa huduma za Afya wanazoendelea kuzitoa.
Akiwa Hanang Waziri Ummy Mwalimu anatarajiwa kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Vituo vya Afya, Zahanati na kuzungumza na watumishi wa Afya.
Aidha Waziri Ummy atatembelea Vituo vya kutolea huduma za Afya ambavyo viliathirika na maafa ya maporomoko ya matope ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 80 pamoja na uharibifu wa miundombinu na mali.