Mchezaji wa Manchester City Erling Haaland amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia wa Wanaume wa IFFHS wa 2023.
Haaland ni mchezaji wa tano tu kupata tuzo hiyo baada ya Marco Van Basten, Lothar Matthaus, Robert Lewandowski, na Lionel Messi.
Hiyo inamaanisha kuwa fowadi mashuhuri wa Ureno Cristiano Ronaldo hajawahi kushinda tuzo hii.
Raia huyo wa Norway alikosa tuzo ya Ballon d’Or licha ya kufunga mabao 52 katika mechi 53 alizochezea Manchester City.
Badala yake, tuzo hiyo ilitolewa kwa Lionel Messi kwa kuiongoza Argentina kutwaa Ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana.
Haaland kwa sasa ni majeruhi lakini anatarajiwa kurejea mwaka mpya.