Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, amesema, Zanzibar inaendelea kushughudia mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa maslahi ya wananchi na taifa.
Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ukumbi wa mitihani skuli ya Bambi shehia ya Bambi, ikiwemo ni miongoni mwa shamrashamra ya kutimia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema miongoni mwa mapinduzi ni kuimarika kwa huduma za Afya, Elimu, Maji safi pamoja na miundombinu ya usafiri, inayotokana na misingi imara iliyo asisiwa na wazee ambapo sasa inatimia miaka 60.
Ameaeema serikali chini ya uongozi wake Rais Dk. Mwinyi, itaendelea kusogeza huduma mbali mbali kwa wananchi wake wote bila ubaguzi wa aina yoyote kama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi.
Amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) una malengo na dhamira za Serikali katika kufanikisha Maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kuinua kipato cha kaya maskini, kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya na Elimu pamoja na kutoa fursa mbali mbali kwa wananchi.
Hivyo, amewataka kuendelea kutumia ukumbi huo kwa lengo lililokusudiwa sambamba na kuendelea kusisitiza ushirikiano wa hali na mali katika ufuatiliaji, usimamizi na utekelezaji wa mradi huu ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu.