Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mfumo wa kodi ulio rahisi kuutumia kwa kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali na kuwafikia walipa kodi wengi zaidi pamoja na kuimarisha ofisi za kodi kila Mkoa na Wilaya zake Zanzibar.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya mwezi wa Shukrani na Furaha kwa mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 29 Disemba 2023.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Yusuph Mwenda kwa kuleta mabadiliko ya utendaji na ufanisi wa kuongezeka ukusanyaji mapato Zanzibar .