Shirika hilo limeeleza kuwa bidhaa zilizoibiwa wiki iliyopita huko al-Jazirah ikiwa ni pamoja na nafaka, mafuta na mboga za majani zingeliweza kutoa msaada wa chakula kwa watu milioni wapatao 1.5.
WFP imesema kuwa vikosi vya RSF vimepora pia lishe maalum 20,000ambazo kwa kawaida hutolewa kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo pamoja na wanawake wanaonyonyesha.
Kundi la RSF linaloongozwa na Mohamed Dagalo limekuwa likipambana na jeshi la Sudan tangu mwezi April mwaka huu (2023).
Operesheni za WFP ni suluhu kwa karibu watu milioni moja waliokata tamaa katika jimbo la Al-Jazirah. Uporaji wa ghala hilo unadhoofisha shughuli hizi wakati ambapo karibu watu milioni 18 nchini Sudan wanakabiliwa na njaa kali.
WFP imesaidia zaidi ya watu milioni 5.6 katika majimbo kumi na saba kati ya kumi na nane kote Sudan kwa usaidizi wa chakula na lishe tangu mzozo huo ulipozuka katikati ya mwezi Aprili 2023. Shirika hilo lilionya mapema mwezi huu juu ya janga la njaa linalokuja ikiwa watu hawataweza kupokea misaada.