Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamtafuta Dereva wa gari lenye namba za usajiri T.301 DPG na tela namba T.562 DNV Lori, Kampuni ya K.T. Abri ambaye ametelekeza gari hilo likiwa na mifuko 30 ya dawa za kulevya aina ya Bhangi yenye uzito wa kg.430.
Akizungumza na waandishi wa Habari akiwa katika eneo la tukio Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro ACP Alex Mkama amesema kukamatwa Kwa watuhumiwa hao ni ushirikiano kati ya jeshi na wananchi
RPC Mkama amesema gari hilo limetokea Iringa kuelekea Dar likiwa limebeba chakula Cha kuku na alipofika katika Kijiji Cha Mangae alipaki gari pembeni mwa barabara kisha kufungua boneti kama anatengenza huku bodaboda sita sikisombelea viroba vya BANGI na kupakia katika gari hilo
Anasema baada ya kupata taarifa hizo walifanya doria na kulikamata gari likiwa katika eneo hilo lakini dereva alikimbia kusikojulika huku madereva wa PIKIPIKI nao wakikimbia na kuacha PIKIPIKI hizo lakini zote zimekutwa hazina namba za usajili.