Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo amependekeza Vyama vyote vya Siasa nchini vipewe rukuzu kwa kuzingatia masharti ili viweze kujijenga.
Zitto ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa mjadala uliowakutanisha Wadau wa Demokrasia nchini kujadili Miswada ya Sheria ya Uchaguzi, Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi ya mwaka 2023.
“Kama mnavyofahamu hivi sasa Vyama vya Siasa vinapata ruzuku kutoka Serikalini kulingana na mapokeo ya kura za Wabunge na idadi ya Wabunge na vilevile idadi ya Madiwani kwa maana hiyo hii inasababisha Vyama ambavyo vinapata ruzuku viwe vichache sana lakini ni muhimu lazima vyama viwe responsible”
“Kwahiyo tunapendekeza kwamba mtaona katika muswada wenu ni kifungu cha 17 ambacho kina ammend kifungu cha 16 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ile amendment iandikwe upya kwa kuweka masharti mapya ya namna ya kugawa ruzuku kwahiyo katika asilimia 100 ya ruzuku ya bajeti ya ruzuku asilimia 10 itengwe kwa ajili ya kugawiwa kwa Vyama vyote kwa usawa ila vyama hivyo viwe vimetimiza masharti ikiwemo Chama kuwa na usajili kamili, pili chama kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na ikathibitishwa kwamba kinakidhi vigezo vya usajili kamili”