KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba wamegawa mitungi ya gesi ya gesi ya Oryx 700 pamoja na majiko yake kwa wananchi na wajasiriamali wakiwemo Baba na Mama Lishe.
Akizungumza leo wakati wa ugawaji wa mitungi huo uliohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Seleman Mwenda, Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Pia amewaomba Watanzania kuyatazama matumizi ya gesi ya kupikia nyumbani kuwa huduma muhimu na mwafaka katika kulinda afya ya jamii. kutu
“Oryx Gas tunaamini ukipika kwa gesi ya Oryx utakuwa unalinda mazingira kwa kuacha kukata kuni na mkaa lakini utakuwa unalinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.
“Wanawake wanatumia muda mchache kupika kwa gesi na hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula” amesema.
Kwa upande wake Seleman Mwenda aliyemwakilishia Dk,Mwigulu amesema jitihada za kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi ya Oryx ni sehemu za kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.
“Kupika kwa gesi kunasaidia kutunza mazingira pamoja na afya hasa kwa baba na mama lishe ambao wanajihusisha na shughuli za upishi kwani tumegundua misitu mingi inateketea kwa sababu ya matumizi ya kupikia”