Jaji Mary Kay Holthus wa Las Vegas nchini Marekani ambaye juzi Jumatano alirukiwa na kushambuliwa na Mtuhumiwa Deobra Redden (30) ambaye alikuwa anajiandaa kumuhukumu, amemtaka Mtuhumiwa huyo afanye afanyavyo bila kukwamishwa na chochote, ahakikishe anafika mbele yake Mahakamani kesho Jumatatu ili amsomee hukumu yake.
Tukio hilo lililotokea Jumatano January 03,2024 lilisababisha kuibuka makelele na taharuki Mahamamani kutoka kwa waliokuwa wanafuatilia kesi huku Jaji akianguka pamoja na bendera pembeni yake na baadaye Watu waliwahi kumuondoa Deobra katika eneo hilo, Jaji huyo alipelekwa Hospitali na baadaye iliripotiwa afya yake ilikuwa salama.
Deobra alikuwa kwenye usikilizwaji wa kesi yake ambayo ilikuwa inatolewa hukumu baada ya mwezi November mwaka jana kukutwa na hatia ya kumshambulia Mtu na kumsababishia madhara makubwa ya mwili.
Mtandao wa Yahoo umeripoti kuwa Deobra ambaye alirudishwa Mahabusu baada ya tukio hilo amenukuliwa akisema “Yule Jaji ni mbaya, mnisamehe kwa kilichotokea na mlichokiona lakini Jaji amenipania”