Wakati vita kati ya Israel na Hamas vikiingia mwezi wake wa nne Jumapili, Januari 7, mkuu wa diplomasia ya Ujerumani Annalena Baerbock, akizuru Jerusalem, alitoa wito kwa Israel kujizuia zaidi, akibaini kwamba “utumiaji wa nguvu zisizo kuwa kubwa zaidi kwa operesheni zake” ulikuwa muhimu.
Jeshi la Israel limesema kuwa “litapigana huko Gaza mwaka mzima” wa 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati akizuru Jordan, baada ya kukutana na rais wa Uturuki siku ya Jumamosi mjini Istanbul, kwa matumaini ya kukabiliana na kusambaa kwa vita kati ya Israel na Hamas katika ukanda mzima.
Jeshi la Israel lilitangaza Jumamosi jioni kwamba “limekamilisha kuvunja muundo wa kijeshi wa Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza” na sasa lilikuwa likizingatia kusambaratisha Hamas “katikati na kusini mwa eneo hili”.
Mkuu wa Majeshi ya Israel (IDF) Herzl Halevi alisema jeshi “litapigana huko Gaza mwaka mzima, hiyo ni hakika,” Gazeti la kila siku la Israel la Ha’aretz limeripoti . Wakati wa tathmini ya hali iliyofanywa katika Kamandi Kuu ya IDF, Halevy amesema mwaka wa 2024 utakuwa mwaka mgumu.
Siku ya Jumapili televisheni ya Al Jazeera ilisema kwamba waandishi wake wawili wa habari wa Kipalestina waliuawa katika shambulio la Israel dhidi ya gari lao katika Ukanda wa Gaza, wakilishutumu jeshi la Israel kwa “kuwalenga” waandishi wa habari wa Palestina. Mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yameonya kuhusu idadi ya waandishi wa habari waliouawa wakati wa mzozo huu, ambayo itakuwa kubwa kupita kiasi hata kwa mzozo. Kulingana na RSF, baadhi ya shahidi zinaonyesha kwamba hiki kilikuwa kitendo cha makusudi, ambacho kimejumuisha “uhalifu mpya wa kivita dhidi ya waandishi wa habari huko Gaza”.