Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza vikwazo dhidi ya makampuni matano ya Marekani kwa kuiuzia Taiwan silaha.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitangaza Jumapili kwamba imeyawekea vikwazo makampuni matano ya masuala ya ulinzi ya Marekani ukiwa ni mjibizo kwa hatua yao ya kuiuzia silaha Taiwan na hatua ya Washington ya kuyawekea vikwazo makampuni na watu binafsi wa China.
Maafisa wa China wanaichukulia Taiwan kuwa sehemu isiyoweza kutenganishwa ya ardhi ya nchi hiyo na daima wamekuwa wakionya dhidi ya hatua za Marekani zinazosababisha mvutano za kuiuzia Taiwan silaha.
China inachukulia hatua ya Marekani ya kuiuzia Taiwan silaha kuwa ni kuingilia masuala yake ya ndani.