Dorival Junior amejiuzulu kama mkufunzi wa klabu ya Sao Paulo ya Brazil ili kuinoa timu ya Taifa ya Brazil, klabu hiyo ilisema katika taarifa Jumapili.
Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) lilitangaza Ijumaa kwamba Fernando Diniz, aliyeteuliwa mwaka jana kwa muda mfupi, amefutwa kazi ili kuajiri kocha wa kudumu kuitayarisha timu hiyo kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026.
Dorival Junior amejiuzulu kama mkufunzi wa klabu ya Sao Paulo ya Brazil ili kuinoa timu ya Taifa ya Brazil, klabu hiyo ilisema katika taarifa Jumapili.
“Klabu ya Soka ya Sao Paulo inatangaza kuondoka kwa kocha Dorival Junior, ambaye ameomba kuondoka kuchukua jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Brazil,” timu hiyo ilisema kwenye taarifa kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter.
Reuters imewasiliana na CBF kwa maoni baada ya shirikisho hilo kutothibitisha mara moja tangazo hilo.
Dorival aliiongoza Flamengo kutwaa taji la Copa Libertadores na Kombe la Brazil mnamo 2022 kabla ya kujiunga na Sao Paulo. Pia amewahi kuzifundisha Atletico Mineiro, Athletico Paranaense, Internacional, Vasco da Gama, Fluminense na Palmeiras.