Mahakama ya kikatiba nchini DRC, inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi ya kupinga matekeo ya uchaguzi wa urais, tarehe 12 mwezi huu.
Ni Kesi iliokuwa imewasilishwa mahakamani na mmoja wa wagombea Theodore Ngoy Ilunga, akitaka matekeo ya uchaguzi wa urais wa disemba 20, kufutwa kwa msingi kwamba ulikumbwa na matatizo mengi ya kiufundi na udanganyifu.
Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi huo tarehe 12 mwezi huu baada ya kuskiza kesi hiyo jumatatu, ambapo upande wa rais Felix Tshiesekedi aliyetengazwa mshindi wa uchaguzi huo kujitetea mahakama pamoja na tume ya uchaguzi CENI.
Afisi ya kiongozi wa mashataka nchini DRC, inataka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo ikisema haina msingi .
Visa kadhaa vya udanganyifu wa kura viliripotiwa katika uchaguzi wa Urais nchini DRC, pamoja na ule wa wabunge na madiwani.