Afisa wa jeshi la wanamaji la Marekani ambaye alikiri hatia ya kutoa taarifa nyeti za kijeshi kwa afisa wa ujasusi wa China alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka miwili jela siku ya Jumatatu, idara ya sheria ya Marekani ilisema.
Wenheng Zhao, 26, na mwanamaji mwingine wa Marekani, Jinchao Wei, walikamatwa mwezi Agosti kwa tuhuma za kufanya ujasusi nchini China.
Zhao alikiri hatia katika mahakama ya shirikisho huko California mnamo Oktoba kwa mashtaka ya kula njama na afisa wa ujasusi wa kigeni na kupokea hongo.
Siku ya Jumatatu alihukumiwa kifungo cha miezi 27 jela na faini ya $5,500.
Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, Zhao, ambaye alikuwa katika kituo cha jeshi la wanamaji kaskazini mwa Los Angeles, alipokea karibu dola 15,000 kutoka kwa afisa wa ujasusi wa China kati ya Agosti 2021 na Mei 2023.
Wenheng Zhao, mwenye umri wa miaka 26, alikiri hatia mwezi Oktoba kwa kupeana taarifa kwa majasusi wa China kwa rushwa.
Zhao alikuwa afisa mdogo anayefanya kazi katika kituo cha wanamaji cha California.
Alipitisha habari kuhusu mazoezi ya kijeshi, maagizo ya operesheni na miundombinu muhimu Kuanzia 2021 hadi 2023, maafisa wa Amerika walisema.