Hali ya taharuki imetanda nchini Ecuador baada ya mmoja wa wakuu wa genge la dawa za kulevya nchini humo kutoroka gerezani.
Adolfo Macias – anayejulikana pia kama Fito – aliripotiwa kutoweka kwenye seli siku ya Jumapili.
Waendesha mashtaka wa Ecuador kisha walifungua mashtaka dhidi ya walinzi wawili wa magereza kama sehemu ya uchunguzi wao kuhusu madai ya kutoroka.
Kiongozi wa genge la Los Choneros alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 34 katika gereza la La Region kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na mauaji.
Kutoroka kwake kulitokea siku hiyo hiyo ambayo alipangiwa kuhamishwa hadi kituo cha usalama cha juu katika jiji la Guayaquil.
Rais Daniel Noboa alitangaza hali ya hatari, ambayo itaruhusu mamlaka kusimamisha haki za raia na kuwapeleka wanajeshi magerezani.
Amri hiyo itafanya kazi kwa siku 60, huku Noboa akisema atakabiliana na uhalifu ndani ya magereza na hatakoma hadi “atakaporejesha amani kwa wananchi wote wa Ecuador”.
Mnamo 2013, Macias alikimbia gereza lenye ulinzi mkali lakini alikamatwa tena wiki chache baadaye. Polisi wanachunguza ikiwa kutoroka kwake hivi majuzi kunafanana na mwongo mmoja uliopita.
Los Choneros ni mojawapo ya mamlaka ya magenge yanayofikiriwa kuhusika na ongezeko la ghasia zilizofikia viwango vipya mwaka jana na mauaji ya mgombea urais Fernando Villavicencio.