Watu wenye silaha waliojifunika nyuso zao wamevamia studioya televisheniikirusha matangazo ya moja kwa moja nchini Ecuador na kuwatishia wafanyakazi waliojawa na hofu.
Wafanyikazi walilazimishwa kulalasakafuni wakati wa matangazo ya kituo cha televisheni cha umma cha TC katika jiji la Guayaquil kabla ya matangazo yamoja kwa moja kukatwa.
Washambuliaji hao baadaye walionekana wakitoka studio, wakiripotiwa kuwa na mateka kadhaa. Polisi wamekamata watu kuhusiana na tukio hilo.
Hali ya hatari ya siku 60 ilianza Ecuador siku ya Jumatatu baada ya jambazi sugu kutoweka katika chumba chake cha gereza.
Haijulikani iwapo tukio katika studio ya TV huko Guayaquil lilihusiana na kutoweka gerezanikwabosi wa genge la Choneros, Adolfo Macías Villamar, au Fito kama anavyojulikana Zaidi katika jiji hilo.
Katika nchi jirani ya Peru, serikali iliamuru kutumwa mara moja kwa kikosi cha polisi kwenye mpaka ili kuzuia machafuko yoyote kuvuka kuingia nchini.
Marekani imesema inalaani “mashambulizi ya kinyama” nchini Ecuador na “inashirikiana kwa karibu” na Rais Daniel Noboa na serikali yake ya Ecuador na iko “tayari kutoa msaada”.