Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Hassan Banga amesema Tumaini Luvanda (35) mkazi wa Dombwela wilaya ya Makete mkoani Njombe aliyeuawa kwa kukatwa na panga vipande na kisha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili, na baadhi ya viungo kutupwa katika mto ulio jirani na nyumbani katika eneo la Kabinda wilayani humo,ameuawa ambapo katika uchunguzi wa awali wameweza kubaini kuwa kulikuwa na mgogoro wa ndoa na mume wake.\
Amesema mara baada ya kumkamata mtuhumiwa Juma Kyando (36) ambaye ni mume wa Tumaini (Marehemu) kwa kuhusika na mauaji hayo wamebaini kuwa familia yao ilikuwa na matatizo ya ndoa kwa muda mrefu ambapo mwanaume amekuwa akinyimwa unyumba huku pia siku aliyoweza kutekeleza mauaji hayo mke wake alichelewa kurudi nyumbani.
“Familia hii ilikuwa na tatizo la ndoa kwa muda mrefu na mwanaume amekuwa akinyimwa unyumba na siku hiyo ya tukio mwanamke aliondoka nyumbani na alichelewa kurudi alipohojiwa na mume wake hakuwa na maelezo mazuri jambo ambalo lilimpandisha hasira mwanaume na kutekeleza tukio hilo,niueleze tu umma mtu huyu tumemkamata na tunakamilisha upelelezi ili tuweze kumifikisha Mahakamani”Amesema Kamanda Banga
Hata hivyo kamanda Banga ameeleza kuwa kwa namna mtuhumiwa alivyokuwa akitekeleza tukio hilo ilionyesha uwezo wake wa kufikiri ulikuwa ni mdogo hali inayowafanya waendelea na uchunguzi wa kidaktari ili kuona kama alikuwa ni mzima wakati akitekeleza tukio hilo