Winga wa Napoli Khvicha Kvaratskhelia hatoweza kuhamia Saudi Arabia, lakini angependa kuhamia moja ya vilabu vinne barani Ulaya, kulingana na wakala wake.
Kvaratskhelia, 22, ana mchango wa mabao 41 katika mechi 68 alizoichezea klabu hiyo na aliisaidia kushinda Serie A msimu uliopita. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Georgia yuko kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya lakini amevutia baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya na huenda akashawishiwa kuhama.
“Napoli waliongeza mkataba wa [Victor] Osimhen, lakini Khvicha hangekubali uhamisho wa kwenda Saudi hata kama angempa euro bilioni,” wakala Mamuka Jugeli aliambia 1TV Sport Georgia. “Kwa mfano, pengine angekubali kuchezea Real Madrid, Bayern Munich, Barcelona au Manchester City.
“Khvicha ana matamanio na malengo tofauti: anataka kufanikiwa, na tayari anafanikisha.”