Siku ya Alhamisi (Jan.11), mawakili wa Afrika Kusini watawaeleza majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa nini nchi hiyo inaishutumu Israel kwa “vitendo na kutotenda” ambavyo ni “mauaji ya halaiki” katika vita vya Gaza.
Ujumbe wa Afrika Kusini huko Hague utaongozwa na Waziri wa Sheria Ronald Lamola na pia utajumuisha maafisa wakuu kutoka ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa na Wizara ya Sheria, Wizara ya Sheria ilisema katika taarifa yake.
“Tumedhamiria kuona mwisho wa mauaji ya halaiki ambayo kwa sasa yanafanyika Gaza,” Lamola alisema.
Wizara ya Sheria ya Afrika Kusini ilisema Corbyn ni mmoja wa “vigogo waandamizi wa kisiasa kutoka vyama vya siasa vinavyoendelea na vuguvugu kote ulimwenguni” ambao wataungana na ujumbe wa Afrika Kusini huko Hague nchini Uholanzi kwa siku mbili za vikao vya awali ambavyo vitaanza Alhamisi.
Kesi ya ufunguzi ya Alhamisi katika mahakama ya ICJ inalenga zaidi ombi la Afrika Kusini la kutaka mahakama hiyo itoe amri za muda mfupi ikiwa ni pamoja na Israel kusitisha kampeni yake mbaya ya kijeshi.