Volodymyr Zelenskyy amesema usitishaji vita nchini Ukraine ungefaidi Urusi pekee.
Moscow ilikuwa na upungufu wa silaha na pause yoyote ingewaruhusu kuongeza usambazaji wao, alisema.
Amesema Urusi inajadiliana kuhusu ununuzi wa makombora kutoka Iran na imepokea zaidi ya risasi milioni moja kutoka Korea Kaskazini.
Kiongozi wa Ukrain, akizungumza nchini Estonia, alitupilia mbali wazo kwamba usitishaji mapigano ungesababisha mazungumzo yoyote ya kisiasa.
Jana, waziri wa Italia alipendekeza kuwa ingawa msimamo wake kuhusu Ukraine haujabadilika, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuanza kuweka mfumo wa mazungumzo ya amani.
Muktadha zaidi kulingana na sky news ni kwamba : Marekani, Ukraine na washirika sita wameishutumu Urusi kwa kutumia makombora ya balistiki ya Korea Kaskazini na kurusha katika mfululizo wa mashambulizi mabaya ya anga dhidi ya Ukraine, kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.