Katika taarifa ya hivi punde ya uwasilishaji katika mahakama ya ICJ mjini The Hague, Afrika Kusini imetoa taarifa ambayo pengine inatoa ufahamu kuhusu jinsi wanavyofikiri Israel itashughulikia kuwasilisha utetezi wake katika kikao cha kesho.
Wakisema kwamba haikuwa ikitumia sana njia ya uwasilishaji wa sauti/vielelezo, timu ya wanasheria ya Afrika Kusini ilisema:
Ombi la Afrika Kusini katika mahakama hii leo limejengwa juu ya msingi wa haki za kisheria zilizo wazi, si picha, na nyenzo za kina zilizo mbele ya mahakama zimepangwa ili kuonyesha kesi kwa ajili ya hatua za muda kulingana na maamuzi ya awali ya mahakama hii.
Afrika Kusini inaendeleza kesi yake kwa msingi kwamba haki za Wapalestina pia zinastahili kulindwa kutokana na ushahidi ambao haujawahi kushuhudiwa mbele yako kama ule wa makundi ya wahasiriwa ambayo mahakama hii tukufu imelinda hapo awali kwa utoaji wake wa hatua za muda huko nyuma.
Nyenzo hii inathibitisha haki na ukiukaji wao ambao Israeli imefanya, na inatenda, vitendo vinavyoweza kutambuliwa kama mauaji ya halaiki.