Mtoto mdogo (9) mwanafunzi wa darasa la tatu wilayani Babati Mkoani Manyara adaiwa kujinyonga na kisha kuacha ujumbe kwa kutumia wino mwekundu akimuomba msamaha Mama yake kwa kufanya kitendo hicho.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Bagara John Konki ameiambia Ayo tv ” Nitukio la kusikitisha mtoto wa miaka 9 kukatisha maisha yake, nilifika eneo la tukio nikakuta baba wa mtoto ameshamtoa kwenye kamba akijaribu Kumfanyia huduma ya kwanza maana mtoto alionekana bado ana joto hivyo akijaribu kumpulizia hewa kama ataweza kupumua wakamkimbiza hospitali lakini ikabainika tayari ameshafariki”
“Mtoto ameacha ujumbe unaosomeka mwambieni Mama anisamehe nimejiua kwasababu ya Bite akamtaja dada yake (Dada wa Marehemu) ujumbe huu ameandika kwa wino mwekundu na ata baba wa Marehemu amethibitisha kuwa huo ni muandiko wa mtoto wake,ata tulipo muuliza huyu dada yake tatizo ni nini akasema hakukuwa na sababu yeyote” Mwenyekiti Konki
Ayo tv imemtafuta Beatrice (Bite)ambaye nayeye Umri wake ni miaka 15 dada wa marehemu ambaye walikuwa pamoja na mdogo wake kabla ya tukio hilo kutokea ambapo amesema “alikuwa amechukua kitu changu(Cookies) nikamuita Brait nani kachukua kitu changu akasema sio mimi, nikamwambia sio wewe kweli? nikamwambia sema kweli Baba akija anaweza akakupiga akasema ni mimi, nikamwambia usirudie tena akasema sawa,ndipo mimi nikaingia chumbani kwa Mama nayeye akasema dada naenda kusoma akaingia ndani,ndipo Baba alipokuja akamtuta ndani amejinyonga” Dada wa Marehemu