Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imewafunga jela watu 15 baada ya kupatikana na kosa la kufadhili ugaidi kupitia biashara haramu ya dhahabu.
Mahakama hiyo imewafunga washukiwa 10 kifungo cha kati ya miaka mitano na minane, wakati wengine watano wakipewa kifungo cha miaka 10 jela.
Mahakama pia iliwaachia huru washtakiwa wengine tisa.
Washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za kuwezesha uhamishaji wa pesa zilizopatikana kutokana na uuzaji haramu wa dhahabu na mawe yenye madini kwenda kwa vikundi vya wapiganaji.
Upande wa washtakiwa umekanusha mashtaka hayo ambapo kupitia kwa msemaji wake, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Kusambaza :