Conor Gallagher huenda akaondoka Chelsea katika dirisha la usajili la Januari, licha ya Tottenham kumtaka , kulingana na jarida la Sun.
Gallagher, 23, amekuwa mchezaji muhimu wa Mauricio Pochettino na amevaa kitambaa cha unahodha katika mechi nyingi msimu huu.
Hata hivyo, uhamisho wake unaweza kuiletea klabu faida ya £50m na hiyo inaweza kuwa muhimu kwa wao kuangukia kikomo cha FFP.
Tottenham wanashinikiza kufanya mpango wa kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uingereza lakini Pochettino anaripotiwa kuamini kuwa kumwachilia kunaweza kusababisha matatizo kwa Chelsea katika kipindi cha pili cha msimu.