Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Iringa Joseph Nzala Ryata amesema chama hicho kinathamini mchango mkubwa wa vyuo vikuu kwani kazi zao nyingi za kisomi zinaelimisha jamii na vinakuwa muarobaini katika kurekebisha maisha ya Watanzania
Ryata ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wapya wa Tawi la UVCCM wa chuo kikuu cha Iringa ambapo pia amewataka wanafunzi wawe wazalendo na nchi yao pamoja na chama na amewataka wanafunzi hao kujua kuwa ofisi zote za tawi katika maeneo mbali mbali ni kuwakumbusha wasomi na wanajamii kuwa kuna serikali ya chama cha mapinduzi .
Ryata ameendelea kuwataka wanafunzi waweze kushiriki kikamilifu katika chaguzi zinazokuja za serikali za mitaa
Vile vile mbunge wa Viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amezitaka taasisi za elimu mkoani Iringa pamoja na shule kuwa zinakuza matumizi ya Teknolojia yaani ( TEHAMA )
Kabati amesema kupitia taasisi yake ya Ritha kabati Trustumezindua mkakati maalumu wa kuhakikisha zinasaidia shule zote za sekondari zinazomilikiwa na serikali katika maeneo mbalimbali kuanzisha maabara na kufungwa mfumo wa TEHAMA