Mwimbaji wa Nigeria, Divine Ikubor, aka Rema, ameapa kushinda tuzo za Grammy mwaka huu licha ya kutoteuliwa katika tuzo za Grammys za 2024, Rema wakati wa ziara yake kwa mfanyabiashara bilionea, Tony Elumelu katika jumba lake la kifahari la Lagos, alidai kuwa angetwaa tuzo za Grammy mwaka huu.
Mwimbaji huyo wa ‘Calm Down’, ambaye alitangamana na familia ya bilionea huyo na kutoa nakala ya kipekee ya albamu na bidhaa zake (Air Rema) kama zawadi, alimthamini Elumelu kwa kusaidia tasnia ya muziki ya Nigeria kila mara.
Akiongea kwenye kipande cha video kilichoshirikiwa kwenye Instastory yake Rema alisema: “Asante kwa kile umefanya na msaada unao kwenye tasnia ya muziki.
Ninashukuru, ina maana kubwa kwangu. Mwaka huu naleta Grammy.”
Sherehe inayofuata ya tuzo ya Grammy itafanyika mnamo 2025.