Wagombea watano wa upinzani katika uchaguzi wa rais wa Jumapili wa Comoro wamesema zoezi la upigaji kura limekumbwa na “udanganyifu” na “kujaza masanduku ya kura” huku Rais Azali Assoumani akiwa imani kwamba atashinda moja kwa moja katika duru ya kwanza na hivyo kuendelea kutawala visiwa hivyo..
Mouigni Baraka Said Soilihi akiwa ameandamana na wagombea wengine wa urais amesema katika taarifa kwamba: “Kama mwaka wa 2019, tunashuhudia udanganyifu katika udaganyifu unaofanywa na Azali Assoumani na ushirikiano wa jeshi.”
Viongozi hao wa upinzani wanadai kuwa tume ya uchaguzi inapendelea chama tawala, suala ambalo tume imekanusha na kusema kwamba zoezi la upigaji kura limekuwa na uwazi.
Uchaguzi wa Comoro umefanyika Jumapili ambapo Rais Assoumani anatarakiwa kupata ushindi kwa wa muhula wa nne wa miaka 5.