Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, idadi ya watu wanaokimbia vita nchini Sudan imepita milioni 7.4.
Ofisi hiyo imesema idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan pia imeongezeka na kufikia 611,000 katika mwezi mmoja uliopita, huku wengi wa wakimbizi wakitokea Gezira na mikoa mingine.
OCHA imesema, kuongezeka kwa mapigano kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) katika maeneo ya katikati na mashariki mwa Sudan kumesananisha ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu.
Pia Ofisi hiyo imesema, ukosefu wa usalama, wizi, urasimu, mtandao dhaifu na mawasiliano ya simu, ukosefu wa fedha taslimu, na uhaba wa wafanyakazi wa kiufundi na kibinadamu vinaathiri usambazaji wa misaada inayotakiwa.