Sir Jim Ratcliffe anatarajia Ligi ya Premia kuidhinisha hatua yake ya kusimamia shughuli za soka ya Manchester United ifikapo “katikati ya Februari” alipokuwa akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uwekezaji wake katika klabu kabla ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Tottenham.
Ratcliffe, 71, alikubali kununua 25% ya United kutoka kwa wamiliki wao wa Kiamerika familia ya Glazer kwa pauni bilioni 1.3, baada ya mazungumzo marefu hatimaye kukamilika kwa tangazo la mkesha wa Krismasi.
Akizungumza na wanahabari Old Trafford, Ratcliffe alisema kuwa dili hilo halitasitishwa kabla ya mwisho wa dirisha la uhamisho la Januari.
“Mapema hadi katikati ya Februari,” Ratcliffe alisema alipoulizwa ni lini alitarajia makubaliano hayo kupitishwa. “Natumai hatutapata chochote kibaya kwenye CV yangu.
“Hii ni mechi ya kwanza kwangu tangu tufike hapa. Nina furaha sana kuwa hapa, lakini siwezi kujibu maswali yoyote kwa kweli.”
Alipoulizwa ni muda gani ametaka kuhusishwa na United, Ratcliffe alisema: “Miaka michache. Imechukua zamu chache kama unavyojua lakini mambo haya yanahitaji kufanywa.
“Nilifika lini kwa mchezo wa kwanza? Nilipokuwa mtoto. Mdogo kabisa. Kumi au kitu, ni miaka 60 iliyopita.”