Duru mpya ya mazungumzo ya kupata kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza na Hamas imepata maendeleo makubwa, duru zilizo karibu na mazungumzo hayo zinasema, jambo linaloashiria kumalizika kwa miezi kadhaa ya mkwamo na kuibua matumaini miongoni mwa jamaa wakati vita hivyo vikipita siku yake ya 100.
Taarifa mpya ziliibuka katika siku za hivi karibuni za mpango wa kuruhusu dawa – kama vile dawa muhimu – kuwafikia mateka, pamoja na kuongezeka kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza.
Siku ya Ijumaa, ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilithibitisha makubaliano hayo, ambayo yanapaswa kuanza kutekelezwa wiki hii. Wazungumzaji kwa sasa wanajadili jinsi ya kupeleka dawa na usaidizi kwa Israel na Hamas.
Takriban mateka 250 walikamatwa na Hamas wakati wa shambulio ambalo halijawahi kutokea kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, kulingana na takwimu za Israel. Angalau 130 wamesalia utumwani.
Familia za mateka zinaendesha kampeni kwa serikali ya Israel kuongeza juhudi za kuwaachilia, zikisema mateka hao walikuwa na afya mbaya, wengine wakiwa na magonjwa tata, wengine majeraha.
Baadhi ya familia zilikusanyika katika eneo karibu na mpaka wa Gaza katika siku za hivi karibuni ili kutangaza jumbe za msaada kwa wapendwa wao kwa kutumia vipaza sauti.