Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza inasema watu 24,285 wameuawa tangu Oktoba 7.
Takwimu hizi haziwezi kuthibitishwa kivyake, na inaaminika kuwa ni pamoja na raia na wanachama wa Hamas waliouawa huko Gaza, ikiwa ni pamoja na matokeo ya makombora ya makundi ya kigaidi.
Jeshi la Israel lilishambulia Hamas siku ya Jumatatu baada ya kundi la wanamgambo wa Palestina kutoa video ambapo lilitangaza kifo cha mateka wawili.
Video hiyo ilionyesha mateka mwanamke anayeitwa Noa Argamani, 26, akizungumza kwa kulazimishwa, akifichua kwamba wanaume wawili aliotekwa nao waliuawa.
Likijibu video hiyo, jeshi la Israel lilisema ni “matumizi ya kikatili ya mateka wasio na hatia.”
Msemaji wa jeshi Daniel Hagari pia alikataa madai ya Hamas kuwa mateka hao wawili waliuawa kwa shambulio la bomu la Israel, kwa kusema kuwa kundi hilo la wanamgambo lilikuwa likidanganya.