Wizara ya Afya imetangaza kufuta matokeo yote ya mtihani wa usajili na leseni wa Wauguzi na Wakunga kwa Watahiniwa wa Stashahada 1330 uliofanyika September 07,2023 baada ya mtihani huo kuvuja na kusambaa kwa Watahaniwa hao.
Wizara imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuhakikisha Baraza linathibitisha Wataalamu wenye sifa stahiki kulingana na taaluma zao kutoa huduma bora za matibabu kwa Wagonjwa pamoja na kuzingatia usalama wa Mteja anayetegemea kupata huduma za Uuguzi na Ukunga.
“Watahiniwa watapewa nafasi ya kufanya mtihani mwingine bila malipo yoyote na hawatahitajika kujisajili tena, mtihani utafanyika tarehe 16/02/2024, Dodoma, taarifa zaidi kuhusu kurudia kwa mtihani huu zitatolewa na Baraza hivyo Watahiniwa wote wanatakiwa kujiandaa na mtihani huo kwa kufuata taratibu kanuni na sheria”
“Mtuhumiwa aliyehusika katika uvujishaji wa mtihani huu tayari amebainika na kusimamishwa kazi huku taratibu kinidhamu na kisheria zikiwa zinaendelea kutekelezwa”